Saturday, March 3, 2012

JUHUDI ZA MKUU WA MKOA WA KAGERA UENDA ZIKAFANIKIWA





 
03.03.2012      JOHN RWEKANIKA          BUKOBA
Juhudi za mkuu wa mkoa wa Kagera Bwana Fabian Masawe za kutunz mazingila kwaajiri ya kusafisha mji zinazoendelea kuzaa matunda ,

Tangu mkuu wa mkoa ateuliwe kuwa mkuu wa mkoa wa kagera pamoja na mambo mengine lakini pia amesimamia zoezi la kusafisha mji kila siku ya Alihamisi 

Juhudi hizi zilienderea kwa wakazi wa manispaa ya BUKOBA baada ya kuu wa mkoa kuongoza maafisa waandamizi na mkuu huyo kuungana na wananchi mtaani akiwa anashiliki shuguli za usafi ,jambo ambalowakazi wa manispaa ya bukoba hawajalizoea .

Mji wa manispaa ya bukoba uko kandokando ya ya ziwa vickitoria ,hivyo karatasi za prastiki zikitupwa ovyoovyo huingia moja kwa moja ziwa vickitoriajambo ambaloni hatari kuleta madhara katika ziwa vickitoria .
Shughuli za kufanya usafi kila Alihamisi haziishi katika manispaa ya BUKOBA tu bali ni zoezi endelevu katika ngazi za wilaya ,kata na vijiji .

Zoezi hili likiendelea linaweza kujenga utamaduni mzuri wautanzaji mazingira nakuweza kuepusha hatali ya mabadiliko ya tabia ya nchi ambavyo kwa mwaka juzi nvua tulizopata katika kipindi cha vuli azikutosha,Jambo ambalo limeperekea wakazi walio zunguka manispaa ya bukoba kukabiliwa na upungufu wa chakula .

Hata hivyo changamoto inayo inayokabili zoezi hili katika ngazi za kata vijiji na vitongoji  bado utekelezaji wake unasuasua kutokana na undaji wa ngazi hizo kutolitilia manani kiutendaji labda nikwakutotambua umuhimu wake ,

Mkuu wa mkoa bwana FABIAN MASAWE amehamia mkoani kagera baada ya kuteuliwa na mheshimiwa raisi kuwa mkuu wa kagera  ambavyo alikuwa mkuu wa wilaya ya KARAGWE ,

Friday, March 2, 2012

mila na desturi za kihaya

 Hii ni "NSIIBA" ambayo ilikuwa silaha kuu ya mwanamke katika ndoa ya mila ya kihaya, enzi ya karne ya 16 hadi ya 20. Kifaa hiki kilitumiwa na mwanamke kujisafisha kabla ya kushiriki tendo la ndoa na mme wake, lakini endapo mke na mume wangegombana, mke akaondoka nayo, ina maana mumewe asimfuate na asimshike ugoni (yaani ameenda jumla hata ukimfuata hawezi kurudi). Kifaa hiki kilikutwa katika jumba la makumbusho la Bukoba Musium eneo la Nyamkazi katika manispaa ya Bukoba.
 Waandishi mbalimbali wa habari wakiwa na mwenyekiti wa Kagera Press Club Bw. John Rwekanika (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika jumba la makumbusho la Bukoba Musium  Machi 1, 2012 , walipolitembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya mafunzo ya Online journalism yaliyofanyika katika manispaa ya Bukoba.
 Hii ni picha ya msonge (Nyaruju) kama ilivyokutwa na waandishi wa habari katika jumba la makumbusho la Bukoba Museum lililoko eneo la Nyamkazi katika manispaa ya Bukoba. nyumba hii ilikuwa ikitumika kuhifadhi familia, mifugo na chakula kwa wakati mmoja.
Mwandishi wa habari Lilian Lugakingira (kushoto) akiwa na mmoja wa waanzilishi wa jumba la makumbusho la Bukoba Musum William Rutta (kulia)