Friday, March 2, 2012

mila na desturi za kihaya

 Hii ni "NSIIBA" ambayo ilikuwa silaha kuu ya mwanamke katika ndoa ya mila ya kihaya, enzi ya karne ya 16 hadi ya 20. Kifaa hiki kilitumiwa na mwanamke kujisafisha kabla ya kushiriki tendo la ndoa na mme wake, lakini endapo mke na mume wangegombana, mke akaondoka nayo, ina maana mumewe asimfuate na asimshike ugoni (yaani ameenda jumla hata ukimfuata hawezi kurudi). Kifaa hiki kilikutwa katika jumba la makumbusho la Bukoba Musium eneo la Nyamkazi katika manispaa ya Bukoba.
 Waandishi mbalimbali wa habari wakiwa na mwenyekiti wa Kagera Press Club Bw. John Rwekanika (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika jumba la makumbusho la Bukoba Musium  Machi 1, 2012 , walipolitembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya mafunzo ya Online journalism yaliyofanyika katika manispaa ya Bukoba.
 Hii ni picha ya msonge (Nyaruju) kama ilivyokutwa na waandishi wa habari katika jumba la makumbusho la Bukoba Museum lililoko eneo la Nyamkazi katika manispaa ya Bukoba. nyumba hii ilikuwa ikitumika kuhifadhi familia, mifugo na chakula kwa wakati mmoja.
Mwandishi wa habari Lilian Lugakingira (kushoto) akiwa na mmoja wa waanzilishi wa jumba la makumbusho la Bukoba Musum William Rutta (kulia)

No comments:

Post a Comment